Femmes du Congo

Ukomo

Campuni ya wanawake wa kongomani kwa kupiganisha ubakaji katika jamuhuri ya KONGO imeanzishwa na wamama wa kongomaini wanaoishi mashariki ya KONGO kwa kuweka mukazo juu ya namna ya kupiganisha ubakaji inchini KONGO.

 

Kabla ripoti mengi kuandikwa na vikundi vya upashaji vya habari, shirika la rahia, vituo vya kigeni na pia inchi mbalimbali, ubakaji unatawanika.  Huduma kwa kusaidia wale waliobakwa, na mwito kwa kupiganisha ubakaji zinaendelea sasa ni zaidi ya miaka mine pasipo tendo kamilifu ya kumaliza ujeuri hizo katika vijiji.

 

Campuni imeanzishwa kutokana na nia ya kutafuta njia kamilifu ya kupiganisha ubakaji na kuwepo na uhakika ya kuwa usaidizi unaoletwa kwa ajili ya wale waliobakwa inawafikia hakika. Kwa hiyo, campuni imeandalia :

 . Utafuti juu ya campuni mbalimbali zilizo andaliwa kwa kupiganisha ubakaji ;

. Kuwekwa kwa mafasirio wazi juu ya kazi mbalimbali zinazofanyika kwa kuhudumia wale waliobakwa ili ijulishwe kwa walewanatumika vijijni kwa kusaidia waliobakwa ;

. Utetezi wazi ili usaidizi iweze kufikishwa vijijini ;

. Kuonesha wazi kazi za vikundi vya wamama zinazo fanyiwa vijini kwa kuwasaidia waliobakwa ;

. Kuwa na uhakika ya kuwa huduma ama usaidizi unaheshimu na kutimiza mahitaji hakika ya waliobakwa ;

. Kuwapa malipizi wale waliotenda ubakaji ;

 

Basi campuni inatoa mwito :

. Kwa vituo vya kigeni, vituo vyote vyenyi kusaidia maendeleo, vikundi vya kigeni visivyo vya serkali kufungua na kuweka vituo vya kukamata mpango ya usaidizi katika vijiji vilivyo jereuliwa zaidi ;

. Kwa vituo vya kigeni,vituo vyote vyenyi kusaidia maendeleo,vikundi vya kigeni visivyo vya serkali kuanzisha na kuendelesha husiano ya kazi na vikundi vya wanawke vijini ;

. Kwa vituo vya kigeni, vituo vyote vyenyi kusaidia maendeleo, vikundi vya kigeni kukubali ya kama vikundi vya wa kongomani visivyo vya serkali (ONG locales), zinahaki ya kushiriki katika baraza za mipango zote sawa na vituo vya serkali na zile za kigeni ;

. Serkali ya KONGO kuhimirisha sheria ya kupiganisha ubakaji, kuongeza mafunzo kwa polici na kuwapa viombo vya kazi wanasheria, na kuwapa wale waliobakwa matunzo inayofaa ;

 

Campuni ni malamiko ya vikundi vyia rahia kutokana na ukosefu wa husiono bora, ukosefu waheshima kwa kazi yao, ukosefu wa usawa katika mahitaji na usaidizi vijijini, matendo yasiyoweza kuendelesha na kuhimirisha kazi za kupiganisha ubakaji vijijini kwa siku nyingi.

 

Navigation